VIZUIZI 12 VYA KUSHEHEREKEA MAULID
Hasan Al-Husayniy Imetafsiriwa na ‘Abdun-Naaswir Hikmany Shukrani ni za Allaah, na rahma zimuendee Mjumbe wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni mbora wa viumbe wote … Ninataka kuweka (wazi) mbele ya msomaji, vizuizi (nukta) vifuatavyo kuhusiana na washerehekeaji wa siku ya kuzaliwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aailihi wa sallam), ikitajwa tendo lao la kufanya hivyo, kwa mujibu wa Shari’ah ya Kiislamu; kitendo cha haki iliyoruhusiwa (Halali) au dhidi ya Shari’ah (Haramu). Kwa maneno mengine, je inastahiki kupatiwa adhabu? Zaidi ninamuomba Allaah, kwamba makala hii kuwa ni yenye manufaa kwa wote. Kizuizi Cha Kwanza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amemtaka Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata yale ambayo Allaah Amemshushia na sio kubuni maelekezo ya ‘uongo’, Anasema katika maneno Yake ndani ya Qur-aan: ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا...