Posts

Showing posts from April, 2012

HATARI YA KUIHAMA QUR`AN

Image
Anasema Allaah سبحانه وتعالى  (( وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا ) ((Na Mtume amesema: Ee Mola wangu! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur-aan ni kitu kilichohamwa (kilichoachiliwa mbali))) [Al-Furqaan: 30] Allaah سبحانه وتعالى Anatuambia jinsi Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alivyokuwa akilalamika kuwa watu wake wameihama na kuipuuza hii Qur-aan. Makafiri Quraysh walikuwa hawataki kusikiliza Qur-aan, na ilipokuwa ikisomwa walikuwa wakizungumza upuuzi au kuzungumza kwa sauti za juu mazungumzo mengine ili wasiisikie  kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى : (( وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لاَ تَسْمَعُوا لِهَذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُون)) ((Na waliokufuru walisema: Msiisikilize Qur-aan hii, na timueni zogo, huenda mkashinda)) [Fusswilat: 26] Hali hii ya kuipuuza Qur-aan vile vile iko miongoni mwa Waislamu hali kadhalika, ingawa Waislamu tofauti yake ni kuwa wameiamini na sio kama Makafiri Q...