WAKATI WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA WAKILIA BOOM,KENYA KWACHAFUKA,WANAFUNZI WAFANYA MAPAMBANO NA ASKARI KISA ONGEZEKO LA ADA
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya wamezua vurugu wakipinga mpango wa serikali kutaka kuongeza karo katika vyuo vikuu vyote vya umma. Polisi walipambana na wanafunzi hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya wanafunzi hao ambao walizua vurugu mjini na kuwapora abiria huku wakiharibu magari ya umma na yale ya abiria katika barabara kuu ya Uhuru katikakati ya jiji la Nairobi. Pia waliripotiwa kuvunja maduka na kuharibu mali ya watu. Wachuuzi walilazimika kuondoka mjini huku polisi wakipambana na wanafunzi hao ambao waliungana kutoka vyuo vikuu mbali mbali kote nchini Kenya. Awali maandamano yao yalikuwa salama ingawa baadaye wanafunzi hao walioanza kuandamana tangu saa nne asubuhi walianza kuzua rabsha na kulazimisha polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya. Wanafunzi hao wanaandamana kupinga mapendekezo ya serikali kuongeza karo ya vyo vikuu , ingawa waziri wa elimu ya juu Profesa Jacob Kaimenyi amesema kuwa serikali bado haijatoa tamko r...