Posts

Showing posts from November, 2014

AJALI MBAYA YA BASI YATOKEA KAHAMA

Image
AJALI MBAYA YA BASI YATOKEA KAHAMA  Hivi ndiyo basi la wibonela lilivyoacha  njia mjini kahama huku ikiwa imelala ubavu             KAHAMA. Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine arobaini kujeruhiwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kutokea ajari mbaya iliyohusha basi la abiri. Tukioa hilo lilitokea jana majira ya saa Kumi na mbili asubuhi katika eneo la Phantom Nje Kidogo mwa mji wa Kahama,wakati basi aina ya Scania lenye no T 412 CGN mali ya Wibonela Ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka. Kwa mjibu wa Mganga Mfawidhiwa Hospitali ya mji wa Kahama Joseph Ngowi alisema walikufa kati yao wanaume ni 3 akiwemo mtoto na mwamke ni Mmoja ambapo aliataja kuwa ni Amina Emmanuel ambaye alikuwa mjamzito mkazi wa Kigoma, Salum ambaye alifahamika kwa jina moja , Mtoto wa miezi mitatu Robin Jordan na mwanamme mmoja mabaye hakufahamika. Aliataja waliojeruhiwa ni Mauld Shab...

SHEREHE YA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA KMA 2014/2015

Image
JUMUIYA YA WAISLAM MKOA WA KILIMANJARO (KMA) INAYOFURAHA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WOTE WA MWAKA WA KWANZA KATIKA JUMUIYA YETU KWA MOYO MMOJA..... TUNAWAPONGEZA KWA KUJA KWENYE SHEREHE NA KATIKA JUMUIYA YETU HONGERENI KWA KUCHAGULIWA KATIKA JUMUIYA YETU

BUNGE LA TANZANIA LAWAKA MOTO

Image
BUNGE LA TANZANIA LAWAKA MOTO Ni kuhusu sakata la ESCRO hasa baada ya mahakama kuleta barua ya kuzuia sakata hilo kujadiliwa bungeni,wabunge wachachamaa na kutaka ESCRO kujadiliwa Naibu spika wa bunge Job Dungai, yeye ndiye kashikilia rungu, Ripoti " ijadiliwe au la" Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali, (PAC), Zitto Kabwe. Taarifa ya CAG kuhusu akaunti nya Tegeta Escrow, iko mikononi mwake Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, (CHADEMA),akizunghumza bungeni mjini Dodoma jana, wakati lile sakata la IPTL, linalogubigwa na akauti iliyojichukulia umaarufu TEGETA ESCROW, lilipoibuka bungen i wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu. Wabunge wanataka "ngoma" ijadiliwe bungeni, licha ya kashfa hiyo kuwa tayari mahakama kuu ya Tanzania Mbunge wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, huyu ndiye aliyeibua kashfa ya akaunti ya Teg...

DONDOO ZA AFYA: UFAHAMU UGONJWA WA EBOLA KWA KINA

Image
 DONDOO ZA AFYA:UFAHAMU UGONJWA WA EBOLA KWA KINA Ugonjwa wa Ebola unasababishwa na Virusi na ni ugonjwa hatari unaoambukiza haraka binadamu na wanyama mwitu (hayawani) kama kima, sokwe, popo, ndege, mijusi, amfibia, na kadhalika. Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi aina ya Ebola Virus ni wa mlipuko. Japokuwa hakuna mazingira maalum ambamo virusi vya Ebola vinapatikana, lakini wataalamu wanasema virusi hivyo vinapatikana kwa mnyama ambaye anapatikana zaidi barani Afrika. Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi nyingi na bado unaendelea kupukutisha maisha ya watu wengi hasa barani Afrika. Matukio ambayo yamethibitishwa kuwepo kwa ugonjwa huo ni katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea, Ghana, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Sudan, Ivory Coast, Uganda na kadhalika.   Ugonjwa wa Ebola daima unasambaa ndani ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya.Hata hivyo, matukio mengine yamekuwa yakitokea nje ya maeneo hayo ...