MAKATAZO YA KISHARI`AH KWA WANAWAKE
Imekusanywa Na: Abu Faatwimah Katazo La Kutokuwa Na Shukurani [Kukanusha] Ihsaan Huu dada yangu Muislamu ni uwanja mwingine wenye hatari kubwa, na kwa bahati mbaya ni kuwa wengi miongoni mwa wanawake kwa masikitiko makubwa wameuingia na kuamua kuwa ni katika sehemu zao za kuishi na kutafuta kuridhiwa au kupewa ruhusa ya kwenda watakapo hata kama ni kwenye maasi na pasipo mridhia Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) . Wanawake wengi siku hizi wanapotaka jambo ambalo wanaelewa kuwa mume hatoridhika nalo au halipendi au hata wakati mwingine hayuko tayari nalo kwa sababu moja au nyingine au hata kama hataki ni haki yake; huwa silaha yao kubwa ya kutaka wakubaliwe walitakako kusema usemi wao mashuhuri na wenye kupendeza katika midomo yao: Sikupata kuiona kheri hata siku moja kutokana nawe; yote kwa kuwa amekataliwa siku hiyo alitakalo au amezuiliwa kufanya alitakalo au kwenda atakapo. Mke ni mwepesi wa kusahau au kujisahaul...