UTWAHARA WA MGONJWA
KHUTBA YA KWANZA Utangulizi Ewe Muislamu, Mola amekuumba na atakupa mitihani, basi utakapopata mitihani hiyo usisahau ibada Yake kama kawaida, tena haswa ibada ya swala. Utwahara wa Mgonjwa na Swala zake Baada ya him i di na swala na salamu, Enyi watu, muogopeni Mwenyezi Mungu kisawa sawa. Ewe muislamu, ujuwe Mola alituafikia, mimi na wewe tupate kheri ya Uislamu na bila shaka, maadamu ni Waislamu tutapata mitihani kila aina, ya siri na ya dhahiri ili tumtambue, tumshukuru na kusubiri. Na ndio Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) akasema katika maana ya Aya: يقول الله جلّ وعلا: {وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّى نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنْكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ ﭨ } [محمد:31] . {{Hakika tutawaonja mpaka tujue waumini wa kweli na wavumilivu miongoni mwenu}}. Mwanafunzi wa Mtume, Suhaib Ar-Rumii amesema kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Ajabu ni ya huyu Muislamu, kwa kuwa kila jambo lake ni nzuri. Akipata la kumfurahis...