IBADA YA ITIKAFU.

IBADA YA ITIKAFU. MAANA YA ITIKAFU: Kilugha neno “Itikafu” lina maana kuu mbili, kama zifuatazo: Kuzuia, na Kukaa. Kisheria “Itikafu” ni: Kitendo cha kukaa msikitini kwa mfumo maalumu uambatanao na nia ya kujikurubisha kwa Allah, kwa kutekeleza ibada mbali mbali. HUKUMU YA ITIKAFU: Itikafu ni ibada ya SUNAH katika wakati wo wote na imekokotezwa sana katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani. Na itikafu kwa upande mwingine inaweza kuchukua hukumu ya UWAJIBU, hii ni iwapo mtu atajiwajibishia mwenyewe. Mtu atakaposema nimenuia kukaa itikafu siku moja au mbili iwapo nitapata mtoto mathalan. Katika mazingira haya itikafu itakuwa imekwisha kuwa wajibu juu yake. Kwa sababu ya msingi usemao:(Kutekeleza nadhiri ni wajibu). Imepokelewa kwamba Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Mwenye kutia nadhiri ya kumtii Allah, basi na amtii”. Bukhaariy DALILI YA ITIKAFU: Ibada hii ya itikafu imethib...