Muswada wa Mahakama ya Kadhi Waondolewa Bungeni
Muswada wa Sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara hautajadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma baada ya serikali kuuondoa kwa maandalizi zaidi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema jana usiku kuwa wameamua kuuondoa muswada huo ili kupata fursa ya kutoa elimu zaidi kwa viongozi wa dini na kuufanyia marekebisho baadhi ya maeneo.Alisema serikali inatarajia kuurejesha tena bungeni mwezi ujao. Hata hivyo, habari za uhakika kutoka Dodoma zinasema kuwa kulikuwa na mvutano mkali ndani ya kamati ya Bunge iliyokuwa inashughulikia muswada huo uliokuwa kwa misingi ya imani hivyo busara ilitumika kuahirishwa uwasilishwaji kwa mara ya pili kwani mjadala kwenye Bunge zima ungeweza kuleta mpasuko. Muswada huo ulikuwa unawasilishwa kutokana na ahadi ya serikali kwenye Bunge Maalum la Katiba ambako mjadala ulikuwa mzito baadhi ya wajumbe wakitaka mahakama ya kadhi iin...