Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Qiyaama hakitosimama mpaka mitetemeko ya ardhi izidi) al-Bukhariy Mengi yameandikwa, mengi tumeyasoma, mengi tumeyasikia. Je, haujafika wakati wa kuamka na kuyazingatia yale ya kutusaidia Siku ya Mwisho? Haijawa bado funzo kwetu kama Qiyama kipo chini ya pua zetu kinasubiri amri tu kije kwetu. Dalili ngapi tushaziona? Dalili ngapi tushazishuhudia? Twasubiri hadi milango ya toba ifungwe ndio turudi kwa Mola wetu? SubhaanaAllaah! Ya Sunami hatuyaoni? yaliyowapata watu Duniani, hadi tukawa mashakani, bado tunamuasi Manani? Tumegeuka ashaddu wa kumuasi ar-Rahmaani, hadi kuwa sawa na nyani? {{ Na bila shaka Tumewaumbia Moto wa Jahannamu wengi katika majini na wanadamu: Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo. Hao ni kama wanyama; hali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. }} [Al-A’araaf: 179] Basi kama ndugu yangu Muislamu unazo nyoyo, fahamu umepewa na macho...