KUMI LA MWISHO LA MWEZI WA RAMADHANI
Mwenyezi Mngu Aliyetukuka Ametuwekea ibada tukufu katika kumi la mwisho la Ramadhani, zenye kuzidisha Imani na kufanya ibada zikamilike na neema kutimia. Ibada hizi ni Zaka za Fitri na Swala ya Idi. Ametuwekea Zaka za Fitri ili zimsafishe mwenye kufungana na maneneo machafu na matendo visivyo faa na ni chakula kwa masikini, na Ametuwekea Swala ya Idi ili kudhihirisha nguvu za Waislamu na umoja wao na vile wanavyo jikusanya pamoja. Lengo la Mada: Kuwakumbusha watu fadhla za siku kumi za mwisho wa Mwezi wa Ramadhan Kubainisha mafundisho ya Mtume katika siku hizi Kuimarisha mafungamano ya mja na Mola wake, nakufanya bidii kujikurubisha kwa Allah Utangulizi Enyi Waislamu, Siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani zinaendelea kuisha. Na hivi karibuni tutaanza kumi la mwisho. Je ndugu yangu Muislamu umejiuliza suali moja; Je nimefaidika kiasi gani na siku zilizopita? Kuwa mkweli na nafsi yako na u...